Wednesday, October 31, 2012

Mbunge Sugu Noma baada ya Bongo fleva sasa ahamia Bongo Movie
Mr Two "Sugu" akikata mistari katika moja ya show
MBALI na kuwa na kipaji cha muziki wa Bongo Fleva, Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ni mkali ile mbaya kwenye tasnia ya filamu na tayari ameshiriki kwenye sinema iitwayo Bifu.

Akiongea jijini Dar es Salaam, Taiya Odero aliye Meneja Uzalishaji wa Papazi Entertainment, wasambazaji wa sinema hiyo alisema, mbali na Sugu wapo mastaa wengine wa filamu pamoja na Farid Kubanda ‘Fid Q anayesumbua kwenye Bongo Fleva.

“Ni filamu ya kipekee, ina hadithi ya kusisimua na wahusika wameweza kukamua vizuri sana. Hapo Sugu ameweka ubunge pembeni na kufanya sanaa, ni kitu kizuri kwa kweli. Sugu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine,” alisema Odero.

Chanzo: Mtandao wa Global Publishers