Wednesday, November 7, 2012

BREAKING NEWS!!!!!!!! OBAMA ashinda uchaguzi Marekani

Rais Barack Obama
 Rais Barak Obama wa Marekani  amepata ushindi mkubwa baada ya kumzidi mpinzani wake Mitt Romney kwa kupata zaidi ya idadi ya kura za Electoral College 303 ambazo ni zaidi ya kura 270 zinatakiwa kupata mtu ili aweze kuwa rais wa Marekani.

 Mitt Romney yeye amembulia kura 206 huku baadhi ya majimbo likiwamo la Florida kura zikiwa bado zinahesabiwa hadi wakati. Hata hata kama zitatoka hazitaweza kuathiri matokeo hayo.

Awali baada ya kushindwa Mitt Romney alimpongeza Obama kwa ushindi alioupata na kumtakia maisha mema.

Alisema alipenda kuwa rais wa Marekani lakini Wamerekani wameamua kumpa urais mtu mwingine yaani Barak Obama.