Monday, November 5, 2012

CCM pigo jingine Arumeru, CHADEMA yatwaa Halmashauri

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa


Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama

Chama cha Mapinduzi CCM huenda ikawa haina chake katika Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),  kwa mara nyingine tena baada ya kushinda ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki sasa imetwaa Halmashauri mpya ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Usa River.

Halmashauri hiyo pia ipo katika eneo la Arumeru Mashariki.

Kwa ushindi huo, CHADEMA sasa wamefanikiwa kuongoza halmashauri ya pili katika Mkoa wa Arusha, kwani kwa zaidi ya miaka kumi wamekuwa wakiongoza Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.

Uchaguzi huo ulifanyika kutokana na Halmasuri ya Arumeru Mashariki kugawanywa, na hivyo kuunda halmashauri mpya ya mamlaka ya mji mdogo wa Usa River.

Kabla ya kugawanywa, mitaa yote ilikuwa ikiongozwa na CCM na hivyo, ikalazimika viongozi hao wajiuzulu ili uchaguzi ufanyike upya wa kuwapata wenyeviti wapya wa mitaa tisa.

CHADEMA kilikuwa kimejizolea ushindi mkubwa katika mitaa sita, huku CCM kiking’ara kwenye mitaa mitatu.Mitaa hiyo na kura zake kwenye mabano ilikuwa Manyata Kati (CHADEMA 118, CCM 78), Nganana (CHADEMA 127, CCM 117), Kisambare (CHADEMA 613, CCM 190), Ngarasero (CHADEMA 785, CCM 355) na Magadini ambako CHADEMA walipata kura 303 dhidi ya 106 za CCM.

Hata hivyo, CCM ilifanikiwa kurejesha mitaa mitatu ya Magadirisho, Mlima Sioni na Usa Madukani.
Kwa ushindi huo, CHADEMA sasa wamefanikiwa kuongoza halmashauri ya pili katika Mkoa wa Arusha, kwani kwa zaidi ya miaka kumi wamekuwa wakiongoza Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.

CHADEMA kimekuwa kikitoa ushindani mkubwa kwa CCM katika Mkoa wa Arusha kwani hata kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki, chama hicho kilitwaa kiti hicho kilichokuwa kikikaliwa na wapinzani wao baada ya aliyekuwa mbunge kufariki.

Source: Mtandao wa Tanzania Daima

No comments: