Saturday, November 3, 2012

IGP apangua Makanda wa Mikoa: Barlow apata Mrithi

Marehemu Liberatus Barlow

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi. 

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Polisi Tanzania Advera Sensa inasema  kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani SACP Ernest Mangu anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza kuziba pengo la marehemu ACP Liberatus Barlow huku ACP David Misime aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya SACP Zelothe Steven anayestaafu ambapo aliyekuwa kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege ACP Ulrich Matei anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani. 

Aidha, wengine waliobadilishwa ni kutoka Makao Makuu ya Polisi na Makao Makuu Idara ya Upelelezi ambapo ACP Engelbert Kiondo kutoka makao makuu Idara ya Upelelezi  anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, ACP Rashid Seif kutoka Makao Makuu ya Polisi Kwenda kuwa Kamanda wa kikosi cha Tazara, ACP Deusdedit Kato kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege.

Wengine ni ACP Shaban Hiki kutoka Kamanda wa Kikosi cha Ufundi kwenda Makao Makuu ya Polisi na ACP Lucas Mkondya kutoka Makao Makuu ya Polisi kwenda kuwa Kamanda wa Kikosi cha Ufundi.
 
Mabadiliko hayo pia yamehusisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa kikosi  cha Usalama Barabarani  ACP Johansen Kahatano anayekwenda kusimamia  Mradi wa SMARTER Traffic ambapo nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa RTO mkoa wa Pwani ACP Swalehe Mbaga.
 
Uhamisho huo pia umewahusisha baadhi ya Wakuu wa Operesheni wa Mikoa, Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia vya Mikoa, Wakuu wa Polisi wa Wilaya na Wakuu wa Upelelezi wa
Wilaya..
 Msemaji wa
Jeshi la Polisi (T).