Sunday, June 30, 2013

Nyanya ya Rais Obama, Bi Sara Obama kuja Tanzania

Rais Barak Obama akiwa na nyanya yake Sara Obama wakati alipomtembelea Kisumu nchini Kenya 
Nyanya wa Rais wa Marekani Sara Obama anatarajiwa kuja Tanzania kuungana na mtoto wake Barak Obama ambaye anafanya ziara Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje imesema imepata taarifa za kuja kwa bibi huyu ambapo imesema haina tatizo kuungana na familia ya Rais Obama kwenye ziara hiyo. Obama anakuja Tanzania na familia yake akiwemo mke wake Mitchelle Obama na watoto wawili wa kike.