Tuesday, November 23, 2010

Rais Kikwete kutangaza Baraza la Mawaziri kesho Novemba 24, 2010


Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atatangaza Baraza la Mawaziri jipya kesho, Jumatano, Novemba 24, 2010.

kwa mujibu wa Idara ya Mawasiliano Ikulu Rais kikwete atatangaza Baraza la Mawaziri hilo jipya kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 31, mwaka huu, 2010.