Monday, July 4, 2011

Membe asema wakuu wa Afrika wataka serikali ya kidemokrasia Libya


Benard Membe Waziri wa Mambo ya Nje

Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Benard Membe amesema wakuu wa nchi za Umoja Afrika waliokutana Malabo Equitorial Guinea mwishoni mwa wiki wameanzia kuutafutia mgogoro wa Libya luhusu ya kudumu.

Katika azimio la wakuu hao wametaka pande tatu zinazopigana ambazo ni upande wa serikali, waasi na majeshi ya NATO zisitishe mapigano mara moja huku wakipendekeza mchakato wa kidemokrasia wa kuwa na serikali iliyochaguliwa na raia wa nchi hiyo na inayoheshimu utawala na sheria na haki za binadamu kuanza mara moja.

wakuu hao wameitaka kamati ya nchi tano iliyoundwa na Umoja wa Afrika kushughulikia mgogoro wa Libya kutekeleza mara moja mpango wa  kukutana na pande zote yaani upande Kanali Muhamar Gaddafi na waasi ili kuangalia ni namna watakavyoanza mchakato wa kufikia maridhiano ya amani.

Kamati ya Umoja wa Afrika inaundwa na nchi za Mauritania, Mali, Afika ya Kusini , Kongo na Unganda.

No comments: