Saturday, August 13, 2011

Kampuni ya BP yafungiwa miezi 3
Kampuni ya BP ambayo ilikuwa ikiagiza na kusambaza mafuta aina ya petrol imefungiwa miezi mitatu kwa kutotii agizo la Mamlaka ya udhibiti wa maji na Nishati nchini Tanzania EWURA ambapo iliagizwa ikiwa na kampuni nyingine kuacha mgomo wa kuuza mafuta lakini ikakaidi agizo hilo.

Hata hivyo vituo vya mafuta vinavyouza mafuta kwa reja reja ambavyo vina majina ya BP havitahusika na adhabu hiyo kwani adhabu hiyo inahusu leseni ya usambazaji mafuta kutoka katika maghala la BP tu.

No comments: