Sunday, September 25, 2011

Simba yaitafuna Mtibwa SugarMchambuliaji wa Simba Emanuel Okwi KUSHOTO akipambana vikali na wachezaji wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Timu ya Simba leo imeitafuna bila huruma timu ya Soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro kwa kuifunga goli 1 - 0 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam nchini Tanzania.

Goli hilo pekee la Simba lilifungwa katika kipindi cha kwanza na mshambuliaji machachari wa timu hiyo raia wa Uganda Emanuel Okwi.

Bofya hapa kulikiliza matangazo ya mprira kati ya Simba vs Mtibwa


Beki wa Simba Nassoro Masoud Cholo  KUSHOTO akijaribu kudhibiti mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Said Rashidi KULIA

Baada ya Goli hilo timu zote zilizinduka na zilianza zilishambuliana kwa zamu lakini ni Simba ndio walioonekana kumiliki kwa kiasi kikubwa mchezo huo katika kipindi cha kwanza.

Mtibwa Sugar walipata nafasi kadhaa ambapo waliweza kulikaribia lango la Simba lakini kutokuwa makini kwa washambuliaji wao walishindwa kupachika mabao.

Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika Simba ilikuwa mbele kwa goli 1 - 0.

Kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa ari mpya baada ya kufanya mabidiliko kadhaa.

Katika kipindi hiki Mtibwa kuingia kwa ari mpya ambapo walionekana mara kadhaa wakilishambulia lango la Simba kama nyuki hata hivyo mabeki wa Simba wakiongozwa na Victor Costa Nampoka waliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Mtibwa wakiongozwa na Tomas Mourice na Masoud Ally.

Hata hivyo Simba nao walichachamaa katika dakika za mwisho ambapo walikosa magoli kadhaa baada ya washambuliaji wake kufika langoni mwa Mtibwa.

Dakika 5 kabla ya mpira kumalizika Simba walipata penati lakini wakashindwa kuitumia nafasi hiyo kuongeza goli la pili baada ya mpiga penati Victor Costa penati yake kupanguliwa na golikipa wa Mtibwa Deogratius Munishi.

Hadi mpira unamalizika matokeo yakawa 1 - 0.

Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kuweka rekodi yake ya kutopoteza mchezo hata mmoja tangu ligi kuu ya Tanzania bara ilipoanza msimu huu.


No comments: