Tuesday, April 2, 2013

Maafa mengine 18 wahofiwa kufa kwenye mgodi Arusha


Askari wa Jeshi la Wanachi wa Tanzania pamoja na baadhi ya wananchi wakiendelea na zoezi la uokaji
Watu zaidi ya 18 wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mgodi wa kokoto za Morrum huko Moshono Arumeru mkoani Arusha.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kwa sasa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wakishirikiana na raia wanaendelea na zoezi la uokoaji na tayari mtu mmoja ameokolewa na miili ya watu watatu imeopolewa.
 

Tukio hili linatokea ikiwa ni siku siku tatu baada ya maafa mengine kutokea jijini Dar es Salaam ambapo watu 36 wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka.

Tutaendelea kufuatilia tukio hili kwa karibu na tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kwa kadri tutakavyokuwa tunazipata
Umati wa wananchi eneo la tukioHuyu aliyebebwa alipoteza fahamu baada ya kuona mwili wa rafiki yake ukifukuliwa

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwasili eneo la tukio


Raia na askari wa Jeshi la Wananchi wakiendelea na zoezi la uokozi


Mwili wa dereva aliyekuwa akiendesha gari lililofukiwa na kifusi baada ya kutolewa