Saturday, July 9, 2011

Mr II "Sugu" akamatwa na Polisi

Mbuge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Mr II)
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarafu Mr II amekamatwa na polisi mkoani Mbeya akituhumiwa kufanya mkutano wa hadhara bila kibali
cha jeshi hilo. Mr ii alikuwa akihutubia mkutano huo ulioandaliwa na chama chake cha CHADEMA katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.
Habari zinasema Mbilinyi alinyimwa dhamana na alikuwa rumande hadi usiku wa kuamkia leo.

Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya jeshi la polisi kuwakamata wabunge na hasa wa upinzani bila kufuata utaratibu. Hivi karibuni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alikamatwa na polisi mjini Dar es Salaam na kukaa rumande kwa siku moja kwa madai ya kuruka dhamana lakini baadae alipofikishwa mahakamani ikabainika hakuwa na kesi ya kujibu.


                                      

No comments: